Katika hali ya kuchekesha, mwizi mmoja nchini China alijikuta akishikwa pabaya alipoamua kulala usingizi katikati ya wizi, jambo lililomfanya mwenye nyumba kuwatahadharisha familia yake na polisi na kukamatwa.
Tukio hilo lilijiri katika mkoa wa Yunnan, ambapo mvamizi huyo aliyetambulika kwa jina la Yang, aliingia katika nyumba moja lakini akashtushwa na sauti, na kumfanya ajihifadhi katika chumba tofauti lakini, baada ya kuvuta sigara, alipitiwa na usingizi na akalala.
Mmiliki wa nyumba hiyo, Tang, awali alipuuzilia mbali mlio huo mkubwa kama kelele kutoka kwa nyumba ya jirani lakini alianza kutilia shaka sauti hizo zilipoendelea na kuongezeka na baada ya uchunguzi, aligundua mgeni asiyetarajiwa, amelala kwa amani sakafuni katika chumba kingine.
Mamlaka zilifichua kwamba Yang alikuwa na historia ya uhalifu, baada ya kufungwa jela kwa wizi mwaka wa 2022.
Akiwa ameachiliwa mnamo Septemba, alianza tena shughuli zake haramu, na hatimaye akamatwe. Kesi hiyo kwa sasa inachunguzwa.