Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema, Treni kwa mara ya mwisho ilifika Arusha mwaka 1986 ambapo ni kama Mwl. Nyerere alipoondoka Madarakani aliondoka na huduma ya Reli.
Ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa safari za Treni kutoka Dar – Tanga – Moshi na Arusha huku mgeni rasmi akiwa ni Rais Magufuli.
Ukarabati wa Reli hiyo umegharimu Tsh. Bilioni 14 ambazo zimetolewa na Serikali. Huduma hiyo imeboresha usafirishaji wa Mizigo na Abiria wa njia ya Arusha kuelekea Dar.