Huu ndiyo utakuwa mwonekano wa Majengo Pacha ya Tanzania Tower jijini Nairobi, Kenya, mara baada ya kukamilika kwake.
Tanzania Tower itakuwa na majengo mawili yenye urefu wa ghorofa 22 kila moja – likitumika kama Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya, makazi na ofisi za kupangisha. Jengo hilo litajengwa na Mfuko wa Hifadhi wa NSSF katika eneo la katikati ya jiji la Nairobi ambalo Serikali ya Tanzania imepewa na ya Kenya kwa ajili ya kujenga ubalozi wake.
Waziri Mkuu wa Kenya, Musalia Mudavadi aliungana na mawaziri January Makamba (Mambo ya Nje)na Deo Ndejembi (Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi na Ajira) katika tukio la uzinduzi wa mradi huo lililofanyika leo.