Zikiwa zimebaki wiki mbili kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kufungua shule leo December 28 2015 Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo ameamua kukutana na watendaji wake ambao ni wakuu wa Wilaya za Mwanza, Wakurugenzi wa Halmashauri, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, wilaya na makatibu tawala wa wilaya na wakuu wengine wa idara.
Ripota wa millardayo.com amenisogezea kilichojiri kwenye setensi za RC Mulongo >> “Mkoa wa Mwanza umekuwa wa tatu kitaifa kwa wastani wa ufaulu 82.14% vijana wote waliofanya mtihani jumla ambao jumla yao 51312 … wanafunzi wote wamepata madarasa ya kidato cha kwanza kwa mwaka 2016, kwa mkoa huu hakuna wanaosubiri kuingia mwezi wa tatu kwa sababu ya upungufu wa vyumba au kwa mazingira yeyote” >> RC Magesa Mulongo.
“Katika mkoa wa Mwanza wilaya iliyoongoza ni Ukerewe imefaulisha kwa 91.03%, Ilemela 89.36%, Nyamagana 85.36% ,Magu 81.39%, Sengerema 78.15%, Misungwi 77.66% na Kwimba 71.71%… kwa hiyo mtaona Ukerewe pamoja na mazingira yake wamewazidi hata Nyamagana, tulidhani watu wa kwanza kutuvusha walikuwa Nyamangana kulingana na mazingira yake wana walimu wengi mazingira safi kila kitu“-RC Magesa Mulongo.
“Na kila mzazi ajue tutakuwa wakali sana kwa sababu tumefanya hawa watoto kufaulu sasa tuhakikishe kila mtoto anaingia shuleni… tunataka kila mzazi na mlezi ampeleke mtoto shule, hamna kisingizio tena… Wakurugenzi toeni maelekezo kwa watendaji wenu wahakikishe kwamba watoro wote wanafatiliwa“- Mkuu wa Mkoa Mwanza, Magesa Mulongo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE