Happy New Year mtu wangu popote ulipo… naomba ikufikie najua watu wangu tayari mmeshapata vitoweo vyenu kwenye hii siku iwe nyama ya ng’ombe, mbuzi, kondoo hata kuku lakini huenda haufahamu idadi ya mifugo iliyochinjwa kwenye machinjio ya nyama Nyakato Mwanza
Nakukutanisha na sentensi za Onesmo Nyamaishwa, Kaimu Afisa mifugo wa jiji anatupa idadi kamili kwenye siku ya mwaka mpya …
“Idadi ya mifugo iliyochinjwa mwaka mpya ni 1,050 kwa mchanganuo ufuatao… Ng’ombe walikuwa 744, mbuzi 138 na Kondoo walikuwa 168… uchinjaji wa siku za kawaida mara nyingi idadi huwa inapungua Ng’ombe 280, Mbuzi na Kondoo kwenye wastani wa 80“- Afisa mifugo wa jiji Mwanza
“Watu wa Mwanza wanakula nyama pamoja na uwepo wa vitoweo vingine kama samaki lakini kwa Mwanza 60% wananchi wanakula nyama… utaratibu wa uchinjaji baada ya ukaguzi wa awali ng’ombe wanakaa masaa 6 hadi 12 uchinjaji unaanza saa 8 usiku hadi saa 12 asubuhi ambapo nyama inatoka kuelekea buchani” Onesmo, Afisa mifugo Jiji Mwanza.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.