Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imeingia kwenye vichwa vya habari mara nyingi wakizungumzia kuhusu dalili za kuwepo mvua kubwa za El Nino, mvua zimeanza kunyesha Dar es Salaam na kwenye maeneo mengine TZ, zinahusiana na El Nino ??!!
Ninazo sentensi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, RPC Charles Mkumbo >>> ‘Leo saa 12 hadi saa 3 asubuhi Mwanza kulikuwa na mvua kubwa maeneo ya Kirumba… dereva wa bodaboda akiwa amewapakia wanafunzi wawili maji yaliwazidi na kwa bahati nzuri wale wanafunzi wanafunzi wawili waliokolewa lakini dereva bodaboda alisombwa pekeyake, mwili wake ulikutwa akiwa amefariki na pikipiki yake imepatikana‘ >>> Kamanda Charles Mkumbo.
Taarifa nyingine ni hii hapa kutoka hukohuko Mwanza >>> ‘Pia tukio la pili, mtoto aitwaye ZAINABU SHABANI mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Nyamanoro alisombwa na maji wakati wakivuka mfereji wa maji, hadi sasa haijafahamika kama amefariki ama ameokolewa. Juhudi za kumtafuta zinaendelea.’ >>> RPC Charles Mkumbo.
Sauti ya taarifa hiyo iko pia kwenye hii sauti kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mwanza.