Mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Jamii FORUMS Maxence Melo amefikishwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam leo kwa mara ya kwanza toka akamatwe na Polisi ambapo amesomewa mashtaka yote yanayomkabili.
Wakili wake Jebra Kambole amesema mashtaka ya Max ni manne ambapo matatu yanafanana ( kuzuia Polisi kufanya kazi yao) na shitaka la nne ni kuendesha mtandao ambao hujasajiliwa Tanzania ( .co.tz)
Baada ya kusomewa mashtaka mshitakiwa aliyakana na upande wa Jamhuri ukasema hauna pingamizi ambapo hata hivyo imeelezwa Max alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo akarudishwa Rumande.
Unaweza kutazama hizi video fupi hapa chini kuona ilivyokua Mahakamani
KUTOKA MAHAKAMANI: Mwanzilishi wa JamiiFORUMS Maxence Melo amerudishwa rumande baada ya kutotimiza masharti ya dhamana katika kosa la nne. pic.twitter.com/J0LQV5QME4
— millard ayo (@millardayo) December 16, 2016
‘Serikali haijazuia matumizi ya mitandao au Intenet kwa Wananchi, kinachozuiwa ni matumizi mabaya’ – Wakili wa TCRA Mahakamani Kisutu leo pic.twitter.com/da7Y5Ny0Bn
— millard ayo (@millardayo) December 16, 2016
Wakili wa Maxence asema mashtaka ni manne, matatu yanafanana (kuzuia Polisi kufanya kazi yao) na la 4 ni kuendesha mtandao bila kuusajili pic.twitter.com/wyYN6J8b05
— millard ayo (@millardayo) December 16, 2016
VIDEO: Chanjo ya UKIMWI yaanza Tanzania, Profesa Ndalichako asitisha ajira za Walimu, tazama hii video hapa chini kupata yote yaliyosomwa na Magazeti ya Tanzania leo https://www.youtube.com/watch?v=aRIYR–Cpqw