Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Fortunatus Muslim amewataka Madereva wote wakiwemo wa Serikali kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kumaliza mwaka.
Kamanda Muslim ametoa kauli hiyo wakati wa operesheni maalum ya nyakua nyakua yenye lengo la kukagua vyombo vya moto katika barabara kuu ya Korogwe na Same.