Leo July 16, 2018 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kwa mwaka wa fedha 2017/18 imekusanya kodi jumla ya Trilioni 15.5 ambayo ni ukuaji wa asilimia 7.5 ukilinganisha na mwaka wa fedha 2016/17 ambayo makusanyo yake yalikuwa Trilioni 14.4
Akitoa taarifa za makusanyo ya kodi Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema sababu zilizopelekea makusanyo hayo kuongezeka ni elimu ya kodi kuzidi kueleweka na walipakodi pamoja na wananchi.
“Katika mwaka wa fedha 2018/19 TRA imedhamiria kutekeleza kwa vitendo kampeni kabambe ya msamaha wa riba na adhabu kwa malimbikizo ya madeni ya nyuma ambapo tunategemea kuongeza urahisi wa kulipa madeni ambayo yalikuwa kikwazo,” amesema Kayombo
Aidha Kayombo amewashukuru walipakodi kwa kuiwezesha serikali kupata mapato hayo yaliyotangazwa leo.
Malalamiko ya RC yamfanya Waziri Mbarawa kumhamisha Mkurugenzi