Ugonjwa wa Myoma ni moja kati ya matatizo yanayoathiri akina mama kuzuia uzazi pamoja na kupoteza maisha, Leo AYO TV inakukutanisha na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye pia ni Daktari Hamisi Kigwangalla akifafanua kwa undani kuhusu ugonjwa huu..
‘Myoma au kwa lugha ya kitaalamu (Uterine Fibroid) ni ugonjwa unaowatokea wanawake wenye umri kuanzia miaka 35 kuendelea, Ugonjwa huu unatokea kwa kujizalisha kwa chembechembe za misuli katika nyumba ya mimba’
‘Myoma huwa haibadiliki kuwa Kansa ugonjwa huu umeonekana kuwapata kwa kiasi kikubwa wakinamama wenye uzito mkubwa au ambao hawajajifungua au wamechelewa kujifungua’
‘Tiba pekee ni kumfanyia mama upasuaji ili kupunguza uvimbe au kuondoa kizazi chote, Wakinamama wengi wanachelewa kuzaa na wengine wanazaa watoto wachache, hii inapelekee wanakuwa kwenye risk ya kupata ugonjwa huu’
Unaweza kuipata yote kwenye hii video hapa chini….
ILIKUPITA HII WABUNGE WANAWAKE WAMJIA JUU WAZIRI KIGWANGALLA BAADA YA MAJIBU HAYA..?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE