Katika kufikia azma ya kuwa na uchumi jumuishi Tanzania iko katika utekelezaji wa mkakati mpya wa matumizi ya fedha kwa mfumo usio wa kibenki ambao umewalenga wakulima wadogo na wakati hususani wanawake ili kuleta usawa wa kijinsia Nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wakati akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa juu kuhusu masuala ya uchumi jumuishi kwa maendeleo uliondaliwa kwa pamoja na Tazania na Uholanzi.
Akizungumza katika Mkutano huo, kando ya mkutano wa 74 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea New York Marekani Prof. Kabudi ameelezea mafanikio ambayo Tanzania imefikia katika mpango wake wa kwanza kuongeza watu katika mfumo wa fedha usio wa kibenki na sasa iko katika mpango wa pili ambapo watumiaji wa mfumo wa fedha usio wa kibenki wameongezeka maradufu.