Profesa Justin Maeda ambaye amefanya kazi sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa msaidizi wa hayati mwalimu Julius Nyerere amesimulia tukio lililotokea nyumbani kwake baada ya watu waliofika nyumbani kwake nakujitambulishwa kuwa ni askari wakidai kwamba awape fedha shilingi million 100 ili waweze kumsaidia baada ya kwenda kwenye eneo lake analofugia nyuki nakukuta pembe ambayo hajajua imetoka wapi.
Maeda anasema alichukuliwa nakupelekwa kituo cha polisi Usa River Mkoani Arusha akiwa na askari hao huku wakimuamuru kutoa shilingi million 200 la sivyo atashtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi ndipo baadaye walimtaka kutoa millioni 100 nakwenda naye benki nakutoa million zaidi ya 70 alizolipwa baada yakustaafu nakuwapa askari ambapo baadaye aliamua kwenda TAKUKURU.
Taasisi yakuzuia nakupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Arusha kupitia kwa mkuu wa taasisi hiyo James Ruge amekiri kuwashilikia askari saba kwa uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo za rushwa.
TAKUKURU ARUSHA YAWASHIKILIA ASKARI SABA KWA TUHUMA ZA RUSHWA “UCHUNGUZI UNAENDELEA”