Leo June 19,2018 tunayo story kuhusu sheria za usalama barabarani ambapo inaelezwa kuwa ni makosa kwa gari la abiria kujaza mafuta sheli huku abiria wakiwa ndani ya gari.
Mwanasheria Leornad Manyama anasema endapo dereva akibainika kufanya kosa hilo anaweza kutozwa faini isiyopungua Shilingi Laki Tatu ama kwenda jela mwaka mmoja.