Kama utakumbuka mwezi uliopita Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo, Nape Nnauye alifanya ziara ya kushtukiza maeneo ya Kariakoo kwenye biashara kubwa ya uuzwaji wa filamu za nje ambazo wauzaji hawakuwa na vibali vya kuuza filamu hizo ambapo zilikamatwa siku hiyo.
Leo August 10 2016 wauzaji wa filamu za nje wakiambatana na mbunge wa Ilala Mussa Azzan zungu walimualika Waziri Nape Nnauye ili kukaa nao kujadiliana kuhusu kuendesha biashara ya kuuza filamu za nje, katika kikao hicho Waziri nape amekanusha habari zilizokuwa zikienea kuwa amezuia uuzwaji wa filamu za nje ndani ya nchi.
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV AUGUST 10 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI