Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Wawakilishi la Ufalme wa Morocco (House of Representatives), Mhe. Rachid Talbi EL ALAMI jijini Rabat, Morocco.
Mazungumzo yao, pamoja na mambo mengine, yalijikita katika kuimarisha uhusiano wa Kibunge baina ya mabunge ya nchi zao, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi hizo.
Vilevile, katika ziara hiyo mhe Naibu Spika amefanya mazungumzo na Rais wa Bunge la Councilors ( House of Councilors) mhe. Naam Miyara, pamoja na Waziri wa Kilimo, Uvuvi, Maendeleo ya Vijijini na Misitu wa Nchi hiyo, Mhe. Prof. Mohammed Sadiki.
Mhe. Naibu Spika yupo nchini Morocco kwa ziara ya kikazi ya siku 5.