Serikali imewataka wakandarasi wanaosimamia ujenzi wa miradi ya maji nchini kuacha siasa na kufanyakazi kwa mazoea.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa maji, Mhandisi Marry Prisca Mahundi wakati akiongea na wananchi wa kata ya Sakura wilayani Pangani mkoani Tanga akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji wilayani humo.
Amewataka Wataalamu hao kuacha kufanyakazi kimazoea kwani wanakwamisha malengo ya serikali ya kuharakisha kuwapelekea maendeleo wananchi wake.
“Wakandarasi achane kufanyakazi kwa mazoea kwenye sekta ya maji tunataka matokeo bora na ya haraka ni wananchi kupata maji Safi na salama ya uhakika,” Mahundi.