Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Uwekezaji ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ngorongoro, amesema amepewa notisi ya siku 30 pamoja na wananchi wengine 45 yakuondoka eneo alilojenga kwenye jimbo lake kwa madai yakujenga kwenye hifadhi ya Ngorongoro.
Ole Nasha amesema wananchi wako tayari kufanya mjadala ambao utakaowawezesha uhifadhi kuwezekana pamoja na shughuli za maendeleo.
“Tuingie kwenye mjadala tuweze kujadiliana na wadau wengine na serikali ili tuweze kupata suluhu,kwa mfano mimi ninapozungumza hapa mimi mbunge na notisi yakuvunjiwa nyumba kwamba naishi kwenye hifadhi”
BAADA YA AGIZO LA RAIS NGORONGORO, WANANCHI WATOA TAMKO “WANAONDOA WATU”