Ni matangazo ya moja kwa moja kutoka Ikulu Dar es Salaam, msafara wa timu ya Yanga wakiitikia mwaliko wa Rais Samia kwa ajili ya kuwapongeza kwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Muda huu katika hafla hiyo anazungumza Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mbunge wa Muheza Hamis Mohamed Mwinjuma maarufu Mwana FA mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuhusu maelezo ya soka na kumpongeza Muwekezaji wa Yanga SC Ghalib Said Mohamed.
“Mheshimiwa Rais tunaendelea kukushukuru kwa kuonesha jitihada Serikali awamu ya Sita katika maendeleo ya michezo na Uboreshaji wa Sekta ya Michezo ndio maana leo hii hauwezi kuzungumzia Mafanikio ya Yanga ya ligi kuu na mashindano ya kimataifa bila kumitaja Kampuni ya GSM ya kaka yangu Ghalib Said ambayo ndio mdhamini mkuu wa Yanga”- Mwana FA
“GSM Iliwekeza na kuwezesha kuwasajili wachezaji mahiri kama Fiston Mayele pamoja na wengineo wengi ambao leo hii wameipa Timu kuwa king’ara katika ligi mbalimbali”- Mwana FA
‘Wachezaji wote wa Yanga walikuwa vitani kweli kweli na Mheshimiwa Rais Yanga hawakufungwa bali wameshindwa kuchukua Kombe”- Mwana FA