Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo imesema itapitia upya makato ya fedha yanayokatwa na taasisi zinazosimamia michezo pindi zinapochezwa mechi zinazoingiza mapato makubwa kama Simba na Yanga na timu mwenyeji iweze kunufaika.
Jibu la serikali limetolewa na naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge Francis Isack Mtinga mbunge wa Iramba Mashariki aliyetaka kujua lini serikali itapitia makato kandamizi katika mambo ya michezo baada ya hivi karibuni mapato ya mchezo wa Simba na yanga kupatikana silingi milioni 450 na timu ya Simba kupata 180.
Akijibu swali hilo mwinjuma amesema “Tutaangalia vilabu vyetu viweze kuendelea kufaidika Zaidi lakini kuna gharama kubwa za taasisi zetu katika uendeshaji wa viwanja na zinaingia gharama kubwa kutoka mifukoni kwao kuifanya michezo hii ifanikiwe kwa hiyo taasisi zetu zitashindwa kujiendesha kama tutazizuia kukata makato yale” Hami Mwinjuma Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo.
Akijibu swali hilo mwinjuma amesema “Tutaangalia vilabu vyetu viweze kuendelea kufaidika zaidi lakini kuna gharama kubwa za taasisi zetu katika uendeshaji wa viwanja na zinaingia gharama kubwa kutoka mifukoni kwao kuifanya michezo hii ifanikiwe kwa hiyo Taasisi zetu zitashindwa kujiendesha kama tutazizuia kukata makato yale”