Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja amewaelekeza Askari wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini kuanza zoezi la kusaka fisi wanaovamia makazi ya watu katika Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.
Masanya amesema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Cecilia Pareso aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuvuna fisi wanaovamia makazi ya watu katika Kata ya Endamarariek Wilayani Karatu
“Tangu mwaka 2019 hadi sasa jumla ya fisi saba wamevunwa na pia Serikali imekuwa ikifanya msako wa fisi mara kwa mara katika maeneo husika niendelee kuelekeza kuanzia sasa Jeshi la Uhifadhi Kanda ya Kaskazini waelekee Karatu wakaanze kufanya msako wa fisi hao ili wananchi waweze kuona umuhimu wa uhifadhi lakini pia fisi hao waweze kurudishwa hifadhini” Mhe. Masanja amesisitiza.”Mary Masanja Naibu Waziri Maliasili na Utalii.