Naibu Waziri wa Sayansi, Ubunifu na Teknolojia wa Uingereza Paul Bristow, ameachishwa kazi katika serikali ya waziri mkuu Rishi Sunak kutokana na msimamo wake wa kuwaunga mkono watu wa Gaza na mpango wa usitishaji kamili na wa haraka wa vita katika mji huo unaoendelea kushuhudia mashambulio na mauaji ya kinyama yanayofanywa na jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Serikali ya Uingereza inafumbia macho jinai za kinyama zinazofanywa na utawala wa Kizayuni huko Gaza na kupinga usitishaji vita katika eneo hilo ikidai kuwa mpango huo utayanufaisha makundi ya muqawama wa Palestina.
Hayo yanajiri licha ya kufanyika maandamano kadhaa makubwa mjini London ya kuunga mkono usitishaji vita huku mashinikizo ya ndani pia kwa vyama vya siasa na serikali ya Uingereza kuzitaka zilaani jinai za Wazayuni yakiwa yanazidi kuongezeka.
Kwa mujibu wa IRNA, msemaji wa ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza alitangaza jana usiku kwamba: matamshi aliyotoa Bristow hayaendani na misingi ya ubebaji dhima kwa pamoja ya viongozi wote wa serikali, na ni kwa sababu hiyo naibu waziri huyo ameuzuliwa wadhifa wake.
Hapo awali, katika barua aliyomwandikia waziri mkuu wa Uingereza, Paul Bristow alikuwa amemwomba Rishi Sunak aunge mkono mpango wa usitishaji wa kudumu wa mapigano huko Gaza.