Naibu waziri wa ulinzi wa Urusi akamatwa kwa tuhuma za kuchukua hongo, kwa mujibu wa chombo kikuu cha upelelezi nchini humo.
Kamati ya Uchunguzi ilisema Jumanne kwamba Timur Ivanov anashikiliwa na uchunguzi unaendelea.
Bw Ivanov aliyeteuliwa katika wizara ya ulinzi mwaka wa 2016, Bw Ivanov, 47, alihusika na miradi ya miundombinu ya kijeshi ya Urusi.
Wanaharakati kwa muda mrefu wamekosoa viwango vya madai ya ufisadi nchini Urusi.
Mnamo 2022, Wakfu wa Kupambana na Ufisadi, kundi lililoanzishwa na marehemu kiongozi wa upinzani Alexei Navalny, lilimshutumu Bw Ivanov kwa kushiriki katika “mipango ya ufisadi wakati wa ujenzi katika maeneo ya Ukraine yanayokaliwa na Urusi”.
Hasa, ilisema alikuwa amefaidika kutokana na miradi ya ujenzi katika mji wa bandari wa Mariupol wa Ukraine, ambao sehemu kubwa yake iliharibiwa na mabomu ya Urusi katika miezi iliyofuata ya uvamizi wa Ukraine.
Tangazo la Kamati ya Uchunguzi kuhusu kukamatwa kwa Bw Ivanov halikuonyesha jinsi naibu waziri huyo alivyojibu madai dhidi yake.
Makosa kama hayo yanaadhibiwa kwa faini kubwa na kifungo cha hadi miaka 15 jela.
Awali, Bw Ivanov alikuwa naibu waziri mkuu wa eneo la Moscow, ambapo waziri wa ulinzi wa sasa Sergei Shoigu aliwahi kuwa gavana kwa muda mfupi, na anasemekana kusalia kuwa mshirika wa karibu wa Bw Shoigu.
Kuzuiliwa huko kunaashiria hatua ya nadra dhidi ya miongoni mwa wasomi wa serikali ya Urusi, ambao wengi wao wanaaminika kutumia nyadhifa zao kujilimbikizia mali nyingi za kibinafsi.
Mnamo 2022, Wakfu wa Kupambana na Ufisadi, kundi lililoanzishwa na marehemu kiongozi wa upinzani Alexei Navalny, lilimshutumu Bw Ivanov kwa kushiriki katika “mipango ya ufisadi wakati wa ujenzi katika maeneo ya Ukraine yanayokaliwa na Urusi”.