Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi David Kihenzile amekiipongeza chuo cha bandari pamoja na bodi ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Nchini TPA kubaki kwenye mühimili sahihi kwenye suala la utoaji elimi yenye kutoa watu wenye utaalamu sahihi kuhudumia bandari nchini.
‘Vyuo vingi vilitoka kwenye muhimili sahihi na kuanza kufundisha mambo ambayo hayapo kwenye misingi iliyofanya kuanzishwa kwa chuo husika iii tu wapate pesa lakini bado TPA pio kwenye stari sahihi naipongeza bodi na watumishi wote’
Naibu Waziri wa uchukuzi Mhe David Kihenzile pia amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini(TPA) za uboreshwaji wa miundombinu zake
‘Ukienda kwenye analysis utakuta wanafuzi kati ya 10,000 wanaosoma kozi zile ambazo ndio msingi wa chuo hawafikii hata asilimia 40 kwamaana yakwamba wanafunzi wengi wanasoma vitu vingine nasio vile ambavyo vitasaidia sekta husika ‘