Kwenye gereza la Kenya kuwepo kwa huyu mzungu huyu ambaye anatumikia kifungo cha muda ni mrefu ni moja ya ishu ambayo imechukua headlines ya story ambazo zimesikika kutoka huko.
Jamaa huyu amefungwa kwenye gereza la Naivasha Kenya, kilichoipa uzito zaidi story hii ni ishu ya kuwepo kwa wafungwa wachache wazungu katika magereza mengi.
Mfungwa huyo anaitwa Joachim alifungwa mwaka 2007 baada ya kukutwa na hatia ya kosa la kukutwa na dawa za kulevya, gerezani ana jukumu jingine ambalo limemuweka kwenye nafasi tofauti na wafungwa wengine.
Jamaa ni engineer wa umeme, gerezani ni fundi wa kutegemewa kwa hiyo ikitokea kama tatizo la kiufundi kwenye masuala ya umeme na vifaa vingine kama TV basi yupo kwa ajili ya kurekebisha kila kitu.
Joachim anasifiwa kuwa na mwenendo mzuri, kapewa sare tofauti na wafungwa wengine pia, unaweza kumcheki kwenye hii video hapa maisha yake ya gerezani kwa ufupi..
Video hii nimeitoa kwenye taarifa ya K24 TV ya Kenya.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook