Ni June 1, 2022 ambapo Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameshuhudia makubaliano ya kibiashara baina ya Shiriki la Posta nchini na Shirika la Posta la nchi ya Oman.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi Waziri Nape Nnauye alisema..’Makubaliano hayo ni ya muhimu na yanaenda kuandika historia ya kukuza uchumi na biashara hasa katika utoaji huduma za kiposta kidigital kati ya Oman na Tanzania na Shirika hilo linabaki kuwa umuhimu mkubwa kwa katika kuwapa Wananchi uhitaji wao’- Waziri Nape
Aidha akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano hayo Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo amesema makubaliano hayo yatasaidia kufanya mageuzi makubwa kwa shirika hilo na kuleta maendeleo makubwa hususani katika biashara.
Miongoni mwa Makubaliano ya pande hizo mbili ni pamoja na kukuza biashara za kidigitali, pamoja na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usambazaji bidhaa mbalimbali zinazo nunuliwa kutoka kwenye mitandao na kusambazwa Afrika Mashariki na kati.