“Ukusanyaji wa kodi ni taaluma lakini changamoto ni kwamba tumeamua kutumia task forces kukusanya kodi, kwasababu sio taaluma yao wanakwenda kuua biashara, wanakwenda kwa Mfanyabiashara hawajali maisha yake ya kesho, tunafurahia matokeo ya kukusanya kodi lakini biashara zinazofungwa ni nyingi, kesho hatuna wa kumkamua maziwa” Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama.
“Kuna sehemu wanakwenda tayari na kesi za uhujumu uchumi, wanawatisha Watu, Watu inabidi watoe fedha na wanafunga biashara zao, tutoke kwenye task force wenye taaluma ya ukusanyaji kodi wafanye kazi yao” Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama.
“Tunatumia kigezo cha idadi ya Wanafunzi kupeleka pesa za Elimu Bure, kigezo hiki nadhani kimepita na wakati, tutanue, Mtu mwenye Watoto 10 na mwenye Watoto 200 baadhi ya mahitaji yanafanana, ukimpelekea Fedha ileile unamuua mwenye Watoto wachache, tuongeze vigezo vya kupeleka fedha” Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama.