Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo, Nape Nnauye amefanya ziara maeneo ya Kariakoo kukagua na kukamata wanaotengeneza ‘kudurufu’ na kusambaza ‘kuuza’ CD ambazo hazina stika kutoka TRA na wala hazikupitishwa na bodi ya filamu kusambazwa kwa wananchi.
Waziri Nape baada ya kukagua maduka hayo amesema kuanzia sasa mtu yoyote atakayenunua CD lazima aulize kama ina stika ya TRA kama haina asichukue na endapo atachukua wote watakua na makosa ya kuhujumu uchumi na watafikishwa katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi, katika zoezi hilo Maduka zaidi ya 40 yamefungwa na bidhaa hizo zimechukuliwa
>>>’Kila anayenunua sasa kazi ya sanaa ambayo haina stika ya TRA naye ni mwizi kwa kama mwizi yoyote sababu ameshirikiana na muuzaji ambaye hajalipa kodi, hata tukikukuta na CD moja haina stika wewe ni mwizi kama mwizi mwingine tutashyghulika na wewe‘ -Waziri Nape
A video posted by millard ayo (@millardayo) on
ULIKOSA SABABU ZINAZOFANYA FILAMU ZA TANZANIA ZISITOBOE KIMATAIFA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI