Satelaiti ya yenye uzito wa Kilogram 272 inatarajia kuangukia Dunia leo April 19,2023 ambapo kwa mujibu wa NASA hatari ya madhara yoyote kumpata Mtu ambaye yupo duniani ni ndogo sana ambapo inakadiriwa ni Mtu mmoja anaweza kuathirika kati ya Watu 2,467.
NASA imesema chombo hicho kilichostaafu cha Reuven Ramaty High Energy Solar Spectroscopic Imager, kinachojulikana kama RHESSI, kitaingia tena kwenye angahewa ya Dunia leo baada ya kukaa zaidi ya miongo miwili katika orbit, ingawa satelaiti nyingi zinatarajiwa kuungua wakati wa kushuka kwake, sehemu nyingine zina nafasi ya kunusurika.
Satelaiti hiyo ilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2002, RHESSI imesaidia kuchunguza na kupima miale ya jua ambayo imewasaidia Wanasayansi kufanya uchunguzi kuhusu fizikia ya mlipuko wa nishati itokanayo na jua, kwa kutumia spectrometer yake ya kupiga picha, RHESSI ilirekodi matukio 100,000 ya X-ray, kulingana na taarifa iliyotolewa na shirika hilo pamoja na picha za gamma-ray.
Satelaiti hii ndio ya kwanza kupiga picha nishati ya juu za miale ya jua, NASA bado haijatoa maelezo yoyote juu ya wapi vipande vya satelaiti hiyo vinaweza kutua wakati huo huo Idara ya Ulinzi ya nchini Marekani na NASA wanaendelea kufuatilia hali halisi.