Katika kipindi cha chini ya saa 24 baada ya kutangazwa kwa ajali ya ndege binafsi ambayo kiongozi wa kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin alikuwemo, na wakati ukimya wa mamlaka umeshuhudiwa nchini Russia, Vladimir Putin amevunja ukimya huo na kuelezea kuhuzunishwa kwake na kifo cha “mtu aliyefanya makosa”.
Rais wa Russia ametoa salamu za rambirambi kwa ndugu wa wahanga wa ajali hiyo.
Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni Putin, anasema wachunguzi wataangalia kilichotokea, lakini hilo litachukua muda.
Aliyeripotiwa kuwa pamoja na Prigozhin kwenye ndege hiyo ni mtu wake wa mkono wa kulia Dmitry Utkin, pamoja na washiriki wengine watano wa Wagner na wafanyakazi watatu.
“Nimemjua Prigozhin kwa muda mrefu, tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990,” Putin anasema katika hotuba yake kwa njia ya televisheni.
Katika kumbukumbu ya wazi ya uasi wa Wagner mnamo Juni, Putin anaendelea: “Huyu alikuwa mtu mwenye hatima ngumu, na alifanya makosa makubwa maishani, lakini pia alitafuta kupata matokeo muhimu, yeye mwenyewe na wakati nilipomtaka kufanya hivyo, kwa sababu za kawaida, kama vile katika miezi hii ya hivi karibuni.”
“Takwimu za awali zinaonesha wafanykazi wa kampuni ya Wagner walikuwa kwenye ndege,” Putin anakiri. “Ningependa kutambua kwamba hawa ni watu ambao wametoa mchango mkubwa kwa sababu yetu ya pamoja ya kupigana na utawala wa UNazi mamboleo nchini Ukraine,” anaendelea.