NI Agosti 11, 2021 mbapo Katibu Mkuu wa CCM, Danile Chongolo amekutana na Waandishi wa Habari akazungumza kuhusu kle kilichoandikiwa kwenye Gazeti la Uhuru kwamba walimnukuu Rais Samia akisema “Sina wazo kuwania Urais 2025”.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu huyo wa Chama amekanusha vikali juu ya taarifa hiyo iliyochapishwa katika gazeti hilo na kutangaza kuwasimamishwa kazi watendaji waliohusika.
“Gazeti la Uhuru ni letu hatuwezi kulikana, maneno yameandikwa kwenye Gazeti letu, nianze kwa kumuomba radhi Rais wetu kwa kumlisha maneno ambayo hajayasema, mahojiano yote ukifuatilia hakuna aliposema yaliyoandikwa kwenye Kichwa cha Habari cha Uhuru leo”- Katibu Mkuu wa CCM
“Asubuhi ya leo niliagiza Bodi ikutane, Bodi imewasimamisha kazi Viongozi ambao wameonekana kuhusika moja kwa moja kwenye shughuli ya uendeshaji, wa kwanza Mkurugenzi Mtendaji Ernest Sungura, wa pili Mhariri Mtendaji na wa tatu Rashid Zahoro ambaye alikuwa Msimamizi wa Gazeti la leo na nimeipongeza Bodi kwa uamuzi wao mzuri”- Katibu Mkuu wa CCM
“Bodi imeunda Tume ya kuchunguza sababu ya hili kutokea na nimewapongeza, pia kwa Mamlaka yangu nimesimamisha kuanzia leo uchapaji wa Gazeti la Uhuru kwa siku saba”-asema Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo.
“Chama cha Mapinduzi (CCM) leo asubuhi kilisema kimesikitishwa na habari iliyoandikwa ukurasa wa mbele ikimnukuu Rais Samia akisema hatogombea Urais 2025 ——> “Sina wazo kuwania Urais 2025” <—— kauli ambayo CCM imesema ni ya uongo kwani Rais Samia hajaongea kitu kama hicho.