Mbunge wa jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham amesema atahakikisha anapambana kutatua changamoto ya vifaa vya mashuleni ili kuinua kiwango cha ufaulu wilayani humo.
Mbunge Salim ameyasema hayo wakati akigawa vifaa hivyo ambavyo aliahidi kwa shule tatu zitakazo fanya vizuri katika matokeo ya mwaka mzima atazipatia Kompyuta na Photocopy Machine ambapo shule zilizopata ni shule za msingi Ilonga,Ng’ongo na Kidugalo ambazo zote zimekabidhiwa vifaa hivyo vyenye thamani ya 11,400,000/=.
Aidha Mhe Salim amewataka walimu wakuu wa shule zote kushirikiana na wazazi kupata fedha kiasi cha 1,500,000/= na yeye atajazia Kiasi kilichobaki atajazia ili kila shule ipate vifaa hivyo.
Kwa upande wa walimu wakuu waliopata vifaa hivyo wamemshukuru Mbunge kwa jitihada zake na wameahidi kuhakikisha wanashirikiana kuondoa changamoto hiyo kwa shule zote wilayani humo.
Wilaya ya Ulanga ina jumla ya shule 86 shule za Msingi 68 na Sekondari 18 ambazo zote zinachangamoto za vifaa hivyo.