Jiji la Nairobi limetajwa kuwa jiji bora kuliko miji yote barani Afrika kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kundi la The Inteligent Community Forum.
Nairobi imeorodheshwa kama moja ya majiji 21 ambayo yanaongoza kwa matumizi ya maarifa ya kisasa ikiwa ni mara ya pili mfululizo na ikiwa ni jiji pekee la Afrika ambalo limeingia kwenye orodha ya majiji haya.
Hata hivyo Nairobi ilishindwa kuingia kwenye orodha ya 7 bora ambapo ilipitwa na miji kama Taipei, Rio De Janeiro, Ipswich iliyoko Australia na Surrey uliopo Canada.
Utafiti huu unafanyika baada ya mapendekezo yanayofanywa na jamii mbalimbali ulimwenguni ambazo hupendekeza miji ambayo inatengeneza wigo mpana wa fursa za kibiashara hasa inayohusisha mtandao wa internet na teknolojia ya kisasa.
Mambo yanayofanya Nairobi iingie kwenye orodha hii ni jinsi ilivyopiga hatua kwenye matumizi ya teknolojia ya uhamishaji wa fedha kwa kutumia mtandao wa simu, sera mbalimbali za Serikali, maendeleo ya mfumo wa Eco yaani Eco System, ushirika uliopo kati ya sekta binafsi na taasisi za elimu ya juu pamoja na uchumi uliotanua wigo wake.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook