Headline za bunge zimeendelea tena leo September 6 2016 ambapo mkutano wa nne wa bunge la kumi na moja umeanza rasmi huku shughuli nzima ikisimamiwa na Spika wa bunge Job Ndugai, katika kipindi cha maswali na majibu moja ya swali lililosikika ni kutoka kwa mbunge wa viti maalum Ritta kabati aliyetaka kujua mpango wa serikali katika kutatua changamoto za askari ikiwemo ukosefu wa nyumba.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba akasimama kutoa majibu ya nyongeza huku akitoa mikakati ya serikali …>>>’Tarehe 9 september kuna wenzetu tuliongea nao kuhusu ujenzi wa nyumba za askari atakuja na kukutana na viongozi husika ili kuanza mkakati huo‘
‘Nimeagiza kila mkoa kufanya tasmini ya kujua wafungwa wenye uwezo wa kufyatua tofali na kutumia bajeti zilizopo kwa ajili ya kuanza kazi ili kupunguza bajeti, Serikali inatambua uzito wa uhitaji wa askari wetu ikiwemo madai ya fedha zao pia‘ –Waziri Nchemba
Unaweza kuendelea kumsikiliza Waziri nchemba kwenye hii video hapa chini..
ULIMIS MAJIBU YA MKURUGENZI NHC KUHUSU MADAI YA KUINGIZA SIASA KWENYE ISHU YA MBOWE HOTELS