February 9 2016 waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi Mwigulu Nchemba alilazimika kusafiri haraka hadi mkoani Morogoro kijiji cha Kambala wilaya ya Mvomero, baada ya taarifa za mapigano ya wakulima na wafugaji kumfikia, safari hii yameingia kwenye headlines nyingine ya kuuwawa zaidi ya mifugo 75 kati ya mifugo 200 waliojeruhiwa kwa mapanga.
Waziri Mwigulu amefika eneo la tukio na kuchukua hatua za haraka kwa kuagiza kamati ya ulinzi ya mkoa na wilaya, kufanya uchunguzi na kuwatafuta wahusika wa tukio la kukatwa katwa mapanga kwa zaidi ya mifugo 75, ili wafike mbele ya mikono ya sheria nakuagiza mahakama kupitia upya hukumu iliyotolewa mwaka 2015 ya kugawa mipaka kati ya eneo la wakulima na wafugaji.
Mwisho waziri Nchemba ameagiza uongozi wa mkoa na wilaya kufanya mkutano wa hadhara wa wakulima na wafugaji tarehe 20/02/2016, ili kuanza harakati za kumaliza mgogoro. Kati ya mifugo inayotajwa ni mbuzi, kondoo na ndama.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE