Vyombo vya habari vya India vimetangaza kuwa serikali ya Kibaniani ya Narendra Modi imeamua kubadilisha jina la nchi hiyo kutoka India na kuwa “Bharat” karibuni hivi.
Serikali ya CNBC India imetangaza kuwa serikali ya nchi hiyo inajiandaa kubadilisha jina la nchi hiyo isiitwe tena India na badala yake iitwe “Bharat.”
Ripoti zinasema kuwa, suala la kubadilishwa jina nchi ya India litajadiliwa na kutangazwa katika kikao maalum cha Bunge kitakachofanyika tarehe 18 mwezi huu wa Septemba.
Vyombo vya habari vya India, vimetangaza kuwa, hata Rais Droupadi Murmu wa India ametumia jina la “Rais wa Bharat” badala ya “Rais wa India” katika barua ya mialiko aliyotuma kwa viongozi wa G20 na hayo ni mabadiliko makubwa ya majina kwenye jukwaa la kimataifa.
Hii ni mara ya kwanza kwa India kutuma mwaliko kwa kutumia “Bharat” na si “India”.
Mkutano wa siku mbili wa kilele wa kundi la G20 utafanyika wiki ijayo Septemba 9 na 10 mjini New Delhi kwa uenyeji wa serikali ya India.