Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ilitoa hadi Jumapili, Agosti 6 saa sita usiku huko Niamey kwa wanajeshi waliompindua Rais Mohamed Bazoum kurejesha utulivu wa kikatiba.
Muda wa makataa tayari umemalizika yapata, wakati ECOWAS ilikuwa imetaja uwezekano wa kuingilia kijeshi ikiwa waasi watang’ang’ania mamlakani na sasa hali ya wasi wasi imetanda nchini Niger.
ECOWAS ilizungumzia kuhusu “operesheni ya kijeshi inayowezekana” na wakuu wake majeshi kutoka jumuiya hiyo walitangaza uwezekano wa kuingilia kijeshi nchini Niger kwa muda wowote baada ya kumalizika kwa makataa ya ECOWAS. Vyanzo vingine vilisema kwamba jeshi la ECOWAS liko tayari.
Lakini haiwezekani kujua kama ECOWAS itachukua mkondo huo, wakati wanajeshi wa Niger walikuwa wameahidi kujihami ikiwa watashambuliwa. Pia ni vigumu kuamua kwa sasa kama kulikuwa na sehemu ya makubaliano katika maazimio ya kambi hizo mbili.
Kwa vyovyote vile, shinikizo ni kubwa kwa ECOWAS. Mali na Burkina Faso, ambazo zinaoongozwa na wanajshi, zilitangaza hivi karibuni kwamba zinatalichukulia shambulio lolote dhidi ya Niamey kama tangazo la vita.
Mataifa yasiyo wanachama lakini yenye ushawishi mkubwa, kama vile Chad na Algeria, yametangaza kwamba yanapinga kabisa uingiliaji kati kwa kutumia silaha.
Licha ya kumalizika kwa makataa yaliyowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), serikali ya Niger haijaonyesha nia ya kumrejesha madarakani Rais Mohamed Bazoum. Jioni ya Jumapili Agosti 6, Baraza la Ulini wa Taifa (CNSP) lilichapisha taarifa kadhaa kwa vyombo vya habari ambazo zinaonyesha shinikizo linaloongezeka kwautawala wa kijeshi.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa Jumapili jioni, CNSP inaeleza kwamba ina taarifa zinazoonyesha kwamba “majeshi ya taifa la kigeni yanajiandaa kushambulia Niger na raia wake”, bila kubainisha ni lipi.
Taarifa nyingine kwa vyombo vya habari inatangaza “kwamba kutumwa kabla ya vikosi vinavyopaswa kushiriki katika vita hivi kumeanza katika nchi mbili za Afrika ya Kati”, tena bila kutaja majina ya nchi hizo. Lakini taarifa hiyo inaongeza kuwa “nchi yoyote ambayo hatua za kijeshi zitaelekezwa dhidi ya Niger itachukuliwa kuwa muasi”.
Kulingana na CNSP, dalili ya kuongezeka kwa shinikizo na, “tishio la kuingilia kati ambalo linazidi kuwa wazi kutoka nchi jirani”, Niger pia imefunga anga yake. Na taarifa kwa vyombo vya habari inaahidi kwamba “ukiukwaji wowote utakuwa somo la majibu ya nguvu na ya papo hapo”.