Moja kati ya habari kubwa za michezo ambazo zimekuwa zikizungumzwa na kujadiliwa sana katika mitandao ya kijamii kuanzia jana February 18 hadi leo ni kuhusiana na Yanga kutosimama kwa dakika moja au kuvaa vitambaa vyeusi mikononi kuomboleza msiba wa mchezaji wa zamani Godfrey Bonny Ndanje.
Kama ambavyo imezoeleka katika soka kiongozi wa soka au mchezaji anapokuwa amefariki, Wachezaji na mashabiki kabla ya mchezo kuanza husimama kwa dakika moja kuonesha heshima au wengine huingia uwanjani wakiwa wamejifunga vitambaa vyeusi mkononi, katika mchezo wa jana wa Yanga na N’gaya hilo halikufanyika.
Kitendo hicho kimejadiliwa sana mitandaoni kiasi cha kufikia mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara kuandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa instagram “Hivi Yanga hawana utu hata kidogo? Geofrey Bonny wameshindwa hata kumpa heshima yake japo kusimama dakika moja? nenda mido tutakulipia jumamosi ijayo“
Ujumbe wa Haji Manara umetafsirika kuwa Simba wao watasimama kuonesha heshima ya mchezaji huyo wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania siku ya Jumamosi ya February 25, katika mchezo dhidi ya wapinzani wao wa jadi Dar es Salaam Young Africans.
FULL HD: All goals N’gaya vs Yanga February 12 2017, Full Time 1-5
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo