Waziri Ndalichako amesema kwa kuzingatia uhitaji wa Wanafunzi waliojiunga na masomo kwa mwaka 2019/2020 pamoja na kwamba katika Bajeti lengo ilikuwa kutoa mkopo kwa wanafunzi elfu 45, lakini hadi kufikia Desemba Serikali ilikuwa imetoa mkopo kwa wanafunzi elfu 49, 485 ambao wamepata mkopo wenye thamani ya shilingi Bilioni 172 na Milioni 400.
Pia Waziri Profesa Ndalichako, ametoa Saa 24 kwa Chuo Kikuu cha DSM kuhakikisha kuwa kinachukua hatua kwa wanafunzi waliotoa tamko ambalo limekiuka taratibu na kutoa taarifa ni hatua gani zimechukuliwa.
MAFURIKO DAR: MKASA WA DADA ALIEZAMA NA IST YAKE MTARONI