Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa Vyuo vya Ufundi Stadi imeendelea kuwekeza katika Vyuo vhivyo huku lengo likiwa ni kuhakikisha kila Mkoa unakuwa na Chuo ifikapo mwaka 2025.
Waziri Ndalichako amesema hayo wakati akizindua Chuo cha VETA, katika Kijiji cha Nyamidaho, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, ambapo amesema katika mwaka wa fedha 2019/2020, Serikali inaendelea na ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi katika Mikoa ya Rukwa, Njombe, Kagera na Geita, kwa gharama ya Shilingi Bilioni 29.8.