Pundamilia kijana anayefahamika kama Ndasiata amezaliwa mapema mwezi Februari katika eneo la Ndasiata, Serengeti akionekana kuwa na upungufu wa madini aina ya Melanin na kumfanya aonekane mweupe kuliko kawaida.
Katika siku za karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la wanyama wa aina hii ambao ni maarufu kama zeruzeru. Miaka ya karibuni alizaliwa Pundamilia mwingine maarufu kama Tira yeye tofauti na huyu ni kuwa kiwango cha Melanin mwilini kilimfanya kuwa na rangi ya udongo na kumpendezesha, kwa sasa Tira anaishi Serengeti, Tanzania ambako ndiko alikozaliwa na kuishi.