Kwa mara ya kwanza katika historia Ndege ya Shirika la Ndege la Air France imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Nyerere Dar es salaam na kumwagiwa maji kama ishara ya kupewa heshima kwakuwa ni mara ya kwanza inatua katika uwanja huo.
Mapokezi ya ndege hiyo yameongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ambapo amesema ndege hiyo itakuwa na route za moja kwa moja mara tatu kwa wiki kutoka Ufaransa hadi Dar es salaam kupitia Zanzibar..
“Haya ni matunda ya ziara ya Rais Dkt. Samia nchini Ufaransa Mwezi February mwaka 2022 ambapo Ufaransa na Tanzania zilikubaliana kudumisha ushirikiano”