Leo September 28, 2018 Ndege ya abiria, Air Niugini aina ya ANG73 kutoka Papua New Guinea, imeshuka kwenye bahari ikitokea uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chuuk huko Micronesia baada ya kukimbia barabara.
Viongozi wa uwanja wa ndege wamesema hakuna abiria yoyote kati ya 35 na wafanyakazi 12 wa ndege hiyo waliopata majeraha makubwa, pia bado chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana na uchunguzi unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Abiria wote katika ndege hiyo ANG73 aina ya Boeing 737 – 800 wamepelekwa hospitalini kwa uchunguzi