Mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi imedungua ndege 19 zisizo na rubani katika Bahari Nyeusi na Crimea na 3 zingine katika majimbo ya Kursk, Belgorod na Orel.
Mashambulizi mapya kwenye ardhi ya Urusi. Jeshi la Kremlin limedungua ndege 19 zisizo na rubani za Ukraineusiku wa Jumatano Septemba 20 kuamkia Alhamisi Septemba 21 juu ya Bahari Nyeusi na peninsula ya Crimea, pamoja na zingine tatu katika majimbo ya Kursk, Belgorod na Orel, Wizara ya Ulinzi imetangaza leo Alhamisi.
“Mifumo ya ulinzi wa anga iliharibu ndege 19 zisizo na rubani za Ukraine juu ya Bahari Nyeusi na eneo la Jamhuri ya Crimea,” wizara imeandika saa nane na dakika 15 kwenye Telegram, na kuongeza kuwa ndege tatu zingine zimedunguliwa katika majimbo ya Kursk, Belgorod (Kusini-Magharibi) na Orel (Magharibi), na kuleta jumla ya idadi ya ndege hadi 22.
Mnamo Agosti 25, chanzo hicho kilidai kwamba Urusi ilidungua ndege 42 za Ukraine huko Crimea, peninsula iliyochukuliwa na Moscow mnamo 2014. Usiku wa Septemba 13 kuamkia 14, Urusi ilisema iliharibu ndege 5 za Ukraine katika Bahari Nyeusi, wakati kikosi cha majini, walipojaribu kushambulia mashua ya doria Sergei Kotov.