Hatimaye serikali ya Malaysia imeachia hadharani data halisi zilizotumika kugundua kuwa ndege iliyopotea ya MH370 ilianguka Kusini mwa bahari ya Hindi.
Data hizo kwa mara ya kwanza zilionyeshwa kwa ndugu na jamaa za abiria waliokuwa ndani ya ndege ambao wamekuwa wakitaka uwazi zaidi kuhusu taarifa hizo kabla ya data hizo kuwekwa hadharani kwa vyombo vya habari.
Nyaraka hizo zilizoachiwa leo, zinajumuisha data zenye takribani kurasa 47 ikiwa ni pamoja na maandishi kutoka kampuni ya Satelite ya Uingereza ya Inmarsat.
Ndege ya MH370 ilipotea Machi 8 mwaka huu wakati ikisafiri kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing.
Ndani ya ndege hiyo kulikuwa na abiria 239 wengi wakiwa raia wa China ambapo hadi sasa haijapatikana na hakuna sababu maalum iliyotolewa juu ya kupotea kwake.
Ungependa taarifa kama hizi zikufikie haraka na kwa wakati? niko tayari kukutumia wakati wowote mtu wangu, jiunge na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.