Kuna watu wangu wengi wamekuwa wakihoji kwamba serikali licha ya kuleta ndege mpya lakini bado hawajaweza kuweka viwango vidogo vya nauli na kusababisha baadhi yao kushindwa kumudu, millardayo.com na Ayo TV leo ina majibu ya maswali hayo kutoka kwa Waziri wa mawasiliano na uchukuzi Prof. Makame Mbarawa.
Waziri Mbarawa amesema…>>>’Unapokuwa na chombo chako cha usafiri ni lazima uangalie gharama zote za uendeshaji pamoja na kuangalia soko lilivyo, hatuwezi kupanga bei ambayo wateja wetu hawawezi kuimudu ‘ –Waziri Mbarawa
‘Leo hii kuna ndege ndogo zinafanya safari za kwenda na kurudi Dar es salaam na Dodoma kwa karibu shilingi laki saba na nusu wakati sisi tunafanya laki tatu na nusu, kwanini watanzania hawazungumzii hilo‘ –Waziri Mbarawa
‘Watanzania wote wajue kwamba serikali imezileta ndege hizi kwa nia ya kuwasaidia na si vinginevyo, na bei zetu zitaendelea kupungua kulingana na ongezeko la wateja wetu‘- Waziri Mbarawa
Unaweza kuendelea kumsikiliza Waziri Makame Mbarawa hapa chini….
ULIIKOSA HII SABABU ZA RAIS MAGUFULI KUHAMIA DODOMA?