Kiungo wa club ya wekundu wa Msimbazi Simba Said Ndemla bado yupo nchini Sweden akiendelea na majaribio yake ya siku 14 katika club ya AFC Eskilstuna ya Sweden, baada ya siku 14 kumalizika majibu yatatoka kama amefuzu au vipi.
AyoTV imefanikiwa kumpata Jamal Kisongo ambaye ni meneja wake lakini Kisongo pia ni meneja wa wachezaji mbalimbali akiwemo Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, Kisongo leo amezungumzia maendeleo ya Ndemla katika majaribio hayo.
“Saidi tumefanya nae mawasiliano jana na kwa sasa wanakwenda mwisho na anafanya vizuri na kwa mazoezi yeye mwenyewe anatia imani ya kufanya vizuri, hata mwenzangu yule wa Sweden amezungumza na mwalimu na kusema amefurahishwa na Ndemla na siku ya Jumamosi anaweza kuwa na mchezo wa kirafiki”>>> Jamal Kisongo
VIDEO: Yanga ilivyoiadhibu Mbeya City leo Chirwa akipiga hat-trick Nov 19 2017