Leo March 21, 2018 Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amesafirishwa kupelekwa mkoani Iringa usiku wa kuamkia March 21.
Wakili wake, Jebra Kambole amezungumza leo March 21, 2018 na kueleza kuwa sasa Nondo yupo Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa.
Tangu Nondo akamatwe hajawahi kuzungumza na wakili wake wala mtu yeyote wa karibu jambo ambalo limekuwa likipigiwa kelele na watu mbalimbali.