Spika wa Bunge Job Ndugai, amewataka wakuu wa Mikoa kote nchini, kuacha tabia yakulewa madaraka na kuonea watu bali wakafanye kazi zao kwakuzingatia misingi ya utawala bora.
Spika Ndugai ameyasema hayo, wakati akifunga mafunzo ya Uongozi yaliyo andaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa Uratibu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, ambapo Jumla ya Wakuu wa Mikoa 26 na Makatibu Tawala wa Mikoa yote 26 wamepatiwa mafunzo hayo kwa muda wa siku tatu jijini Dodoma.
“Kasimamieni Sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma, msiende kumuonea mtu, kawatumikieni matajiri na masikini bila kujali uwezo wao wa kifedha,” Spika Ndugai.
Ndugai, amewataka viongozi hao kutoruhusu urasimu na badala yake wawe watu wanaopatikana iii wananchi waweze kuwafikia kwa urahisi kufikisha kero zao, kwakuwa wao kama wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala, jukumu lao kubwa nikuangalia hali ya Usalama katika Mkoa, hivyo katika Mikoa ipo Migogoro mingi, na suluhu pekee ni kwa kuwasikiliza watu wanao waogoza.
Katika hatua nyingine, Ndugai, amewataka viongozi hao kwenda kusimamia rasilimali za umma kwa weledi, na maarifa walionayo pamoja na kudumisha mahusiano mema.
“Nendeni Mkadumishe mashirikiano baina yenu pamoja na taasisi zingine zote mnazo shirikiana nazo kwa namna moja au nyingine, epusheni migongano ya ninyi kwa ninyi katika maeneo yenu,” Ndugai.
RAIS SAMIA ALIVYOFIKA UWANJA WA MKAPA KUTAZAMA GAME YA SIMBA NA YANGA