Ndugu watatu wa Uganda, Innocent Mugabi, Moses pamoja na Jeremih wametengeneza Ndege ndogo waliyoipa jina la SKY BOY ambayo ipo kwenye asilimia 95 za matengenezo kabla ya kujaribiwa kupaa.
Ndege hiyo imetengenezwa nyuma ya nyumba na wala sio kiwandani, mapenzi yao kwenye sayansi ya kutengeneza Ndege ndio yamesababisha kutengeneza Sky Boy, kwa sasa Ndege hii ina kila kitu kinachoiwezesha kupaa ila kuna vitu vidogovidogo vimebaki vya kumalizia.
Kwa mujibu wa DW Kiswahili, Uganda ni moja ya Nchi ambazo zimetenga mamilioni ya pesa kwa shughuli maalum ya kuwafadhili Wavumbuzi wake wote kama hawa.
MFUGA MBWA: “NILIANZA KUUZA MBWA KOKO, SASA NAMILIKI GARI LA MILIONI 45, FUSO MBILI”
MAISHA YA KAREN MTOTO WA GARDNER, LADY JAYDEE ALICHOMWAMBIA BAADA YA KUMGUNDUA NA MENGINE