Tukiwa bado kwenye headlines za Uchaguzi 2015, taarifa kutoka tume ya Uchaguzi NEC imesema imepokea rufaa za wabunge na Madiwani wa Halmashauri.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa huduma za kisheria wa tume ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe akizungumza na ripota wa millardayo.com alisema..’Ni kweli tume ya uchaguzi ilipokea rufaa ya wabunge na madiwani na zimezifanyia maamuzi katika vikao mbalimbali kilianza tarehe 31, kikafanyika tarehe tena 1, 2 na baadae kikafanyika tarehe 5 kwa hiyo imeziamulia rufaa za wabunge 49 zingine unakuta kwamba walirudia kuleta mara mbili kwa hiyo waliziamulia zikabaki rufaa kama mbili tu za wabunge ambazo zinasubiri taarifa na maelezo kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi’ – Emmanuel Kawishe
‘Kwa upande wa Madiwani mpaka kufikia juzi zilikuwa zimeshaamuliwa rufaa zaidi ya 160 kwa hiyo sasa hivi tunazo kama 30 ambazo vielelezo tumeshapokea na tunaendelea kuandikia na hivi punde tume itaendelea kuzitoa ili wananchi waweze kujua hatima ya yale ambayo wanataka tume kuamulia kwa misingi ya rufaa’- Emmanuel Kawishe
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Emmanuel Kawishe
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos